Makuu yanamsubiri Van Persie

Imebadilishwa: 16 Agosti, 2012 - Saa 11:30 GMT
Robin Van Persie

Robin Van Persie

Aliyekuwa kocha wa klabu ya Tottenham, Harry Redknapp, amebashiri kuwa Robin van Persie huenda akafunga mabao ambayo yatasaidia Manchester United kunyakuwa kombe la ligi kuu ya Premier nchini Uingereza.

Mcheza kiungo wa Manchester United, Michael Carrick, vile vile anatarajia klabu hiyo itashinda vikombe vitatu msimu huu kama ilivyofanya mwaka wa 1999, kwa usaidizi wa Van Persie.

Arsenal, ilikubali kumuuza mshambulizi wake nyota wake mwenye umri wa miaka 29, kutoka Uholanzi, siku ya Jumatano kwa kitita cha pauni millioni 24.

Akiongea NA BBC, Redknapp, amesema, Manchester United ina nafasi kubwa ya kushinda ligi kuu, kufuatia usajili huo wa Van Persie.

Kocha huyo ambaye aliacha kazi mwezi Juni mwaka huu, aliongeza kuwa'' huenda van Persie akawa suluhisho la matatizo ya Manchester United''

Kwa upande wake Carrick amesema kutokana na ufanisi wake msimu uliopita, Manchester United sasa imepata nguvu mpya.

Van Persie alifunga mabao 44 baada ya kucheza mechi 57 kwa klabu yake na taifa lake, yakiwemo mawili dhidi ya Manchester United.

Kabla ya kusajiliwa na Manchester United, van Persie alikuwa na msimu mmoja na klabu ya Arsenal, kabla ya kandarasi yake kukamilika, na kabla ya kumalizika kwa msimu uliopita, alikuwa amedokeza kuwa hataki kuongeza muda wa kandarasi yake na Arsenal.

Van Persei alisajiliwa na Arsenal mwaka wa 2004 kwa kitita cha pauni milioni mbili nukta saba tano na tayari amezionya vilabu vingine vinavyoshiriki kwenye ligu kuu ya premier kutarajia upinzani mkali msimu huu.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.