Kazi yakoma mgodi wa Lonmin

Imebadilishwa: 20 Agosti, 2012 - Saa 18:43 GMT
Wafanyikazi wa Lonmin

Wachimba migodi waliofika kazini lakini pasipo kufanya kazi

Wafanyikazi wa migodi nchini Afrika Kusini wameanza kurudi mmoja mmoja katika migodi ya dhahabu nyeupe, platinum, ambako polisi waliwafyatulia risasi wenzao na kusababisha vifo vya watu 34 Alhamisi iliyopita.

Hata hivyo idadi ya wachimba migodi hao haijatosha kiasi cha shughuli za uchimbaji migodi kuendelea kikamilifu.

Kampuni ya Lonmin ilitangaza kwamba imeanza tena shughuli zake, lakini ukweli ni kwamba ni chini ya thuluthi moja tu ya wafanyakazi waliofika katika migodi, na kazi haijaanza.

Kampuni pia ilitangaza kwamba imetenga muda wa wafanyakazi wote kurudi kazini, na kuongezea muda huo hadi Jumanne.

Imetisha kwamba watakaoshindwa kufanya hivyo, basi watafutwa kazi.

Rais Jacob Zuma alitangaza wiki nzima ya maombolezi kufuatia vifo hivyo vya wachimba migodi.

Vile vile alitaka uchunguzi kamili kufanyika.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.