Lonmin kutowafukuza waliogoma mgodini

Imebadilishwa: 21 Agosti, 2012 - Saa 12:12 GMT
Wafanyakazi wa mgodi wa Marikana walipogoma

Wafanyakazi wa mgodi wa Marikana walipogoma

Kampuni ya madini ya Lonmin imeondoa tishio lake la kuwafukuza kazi wafanyakazi wa mgodi walioshindwa kurejea kazini katika mgodi kufuatia mapambano na polisi wiki iliyopita.

Uamuzi huo umekuja baada ya serikali kuitaka kampuni kuondoa tishio lake kuwafukuza kazi wafanyakazi wake iwapo wangeshindwa kumaliza mgomo wao siku ya Jumanne.

Wiki iliyopita polisi iliwauwa wachimba migodi 34 kwa risasi katika mgodi wa madini meupe yaani Platinum wa Marikana.

Bunge la Afrka Kusini linajadili mauaji hayo siku ya Jumanne kufuatia malalamiko ya wananchi nchini humo.

Rais Zuma ametangaza wiki moja ya maombolezo ya kitaifa na ameahidi kuunda tume itakayochunguza mauaji hayo.

'Kutuliza hisia'

Makamu rais wa Lonmin, Mark Munroe, amesema kuwafuta kazi maelfu ya wafanyakazi Lonmin haitakuwa suluhisho.

"Sifikirii kama italeta suluhisho imara iwapo Lonmin itakuwa ikiweka masharti kulazimisha wafanyakazi kurejea kazini na kusema tutamfukuza kila mmoja iwapo hatawatarejea kazini," amesema.

Polisi wakiwafyatulia risasi wafanyakazi wa mgodi

Polisi wakiwafyatulia risasi wafanyakazi wa mgodi

Waziri mmoja katika ofisi ya Bwana Zuma Collins Chabane, amesema Lonmin imekubali kusitisha masharti yake kwa ajili ya mazungumzo na serikali.

''Nafikiri tunahitaji kutuliza hisia na hasira pande zote na kujaribu kutafuta suluhisho linalofaa katika tatizo hili" amesema katika kituo cha radio nchini humo kwa muhimu wa shirika la habari la AFP.

Lonmin imesema asilimia 33 ya wafanyakazi wake walihudhuria kazini siku ya Jumanne, linaripoti shirika la habari la Afrika Kusini, SAP.

Wajumbe wa ngazi ya juu wa chama cha upinzani walitembelea mgodi huo katika jimbo la Kaskazini Magharibi kabla ya kuanza kwa kikao maalum cha bunge kujadili mauaji hayo, magazeti ya Mail na Guardian nchini humo yanaripoti.

"Tumesikiliza malalamiko ya wafanyakazi na tumejionea wenyewe mazingira halisi. Kwa hiyo sasa tunaweza kuuliza maswali sahihi bungeni, kiongozi wa chama cha United Democratic Movement (UDM) Bantu Holomisa amekaririwa akisema.

Wafanyakazi 3,000 wa mgodi huo waligoma wiki iliyopita kudai malipo bora zaidi kazini.

Mgomo huo ulitamkwa kuwa ni kinyume cha sheria na kampuni ajiri ya Lonmin ambayo ni ya tatu kwa ukubwa duniani katika uzalishaji wa madini meupe yaani platinum.

Wafanyakazi wanaolipwa mishahara kati ya randi 4,000 na 5,000 (sawa na dola za kimarekani kati ya 484 na 605) kwa mwezi, wanasema wanataka mishahara yao iongezwe kufikia randi 12,500 (sawa na dola 1,512).

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.