QPR kumsajili Carvalho kwa mkopo

Imebadilishwa: 22 Agosti, 2012 - Saa 12:36 GMT
Dawson akijaribu kumzuia Wayne Rooney

Dawson akijaribu kumzuia Wayne Rooney

Klabu ya Queens Park Rangers imeingia mkataba na klabu ya Real Madrid ambao utamruhusu mchezaji Ricardo Carvalho kujiunga na QPR kwa mkopo msimu huu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34, na mchezaji kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Ureno, anatarajiwa kujadiliana na klabu hiyo kuhusu malipo yake katika muda wa saa 48 zijayo.

Hapo jana QPR ilimsajili Michael Dawson kutoka kwa klabu ya Tottenham kwa kitita cha pauni milioni saba nukta tano.

Kocha wa klabu hiyo Mark Huges, ameimarisha kikosi chake kufuatia kipigo walichopewa na klabu ya Swansea cha mabao matano kwa yai wakati wa mechi yao ya ufunguzi wa ligi kuu msimu huu, siku ya Jumamosi.

Hata hivyo hakuna mkataba ambao umetiwa saini lakini, QPR inatarajia kuwa usajili huo utakuwa umekamilika kabla ya mechi yao dhidi ya Norwich siku ya Jumamosi.

Usajili wa Dawson, unakaribia kukamilika, huku mchezaji huyo akitarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kiafya kabla ya kusaini mkataba wake.

Dawson amefahamishwa kuwa hatakuwa miongoni mwa wachezaji wa kwanza kumi na mmoja msimu huu.

Inakisiwa kuwa usajili huo utaigharimu timu ya QPR kitita cha pauni milioni tisa.

Klabu ya Nottingham Forest itapokea asilimia kumi ya fedha hizo za usajili, kufuatia mkataba uliosaniwa mwaka wa 2005 wakati ilipomuuza mchezaji huyo.

Carvalho alikuwa mmoja wa wachezaji wa kutegemewa na klabu ya Chelsea na alishirikiana na mcheza kiungo mwingine wa Chelsea, John Terry kuisadia klabu yao kushinda kombe la ligi kuu ya Premier mwaka wa 2005 na 2006 chini ya kocha Jose Mourinho.

Ikiwa usajili huo utafanikiwa, Carvalho ataungana na mchezaji mwingine wa zamani wa Chelsea, Jose Bosingwa katika klabu hiyo ya QPR.

QPR imepangiwa kuchuana na Chelsea tarehe Kumi na Tano mwezi ujao katika uwanja wa Loftus Road.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.