Chelsea kileleni mwa ligi ya England

Imebadilishwa: 23 Agosti, 2012 - Saa 09:47 GMT
Fernando Torres wa chelsea na Kipa wa Reading

Fernando Torres wa chelsea na Kipa wa Reading

Mcheza kiungo wa Chelsea Gary Cahill amekiri kuwa huenda mshambuliaji wao Fernando Torres, alikuwa ameotea, wakati alipofunga bao la tatu, katika mechi ya jana usiku ambapo Chelsea ilishinda Reading kwa mabao 4-2.

Torres alifunga bao hilo baada ya kupata pasi kutoka kwa Ashley Cole na kuiweka Chelsea mbele kwa mabao 3-2, lakini kocha wa klabu ya Reading Brian McDermott amesisitiza kuwa Torres, alikuwa amejenga kibanda katika eneo lao.

McDermott, ambaye alimkabili msaidizi wa refa baada ya mechi hiyo kumalizika, amesema amehuzunishwa sana kutokana na kosa alilolifanya msaidizi huyo wa refa.

Chelsea nusura ishindwe na Reading katika uwanja wao wa nyumbani licha ya wao kufunga kwanza wakati wa mechi hiyo kupitia kwa mchezaji Frank Lampard.

Reading ilisawazisha kupitia kwa mchezaji Pavel Pogrebnyak kabla ya Danny Guthrie kufunga la pili.

Gary Cahil naye akaifungia Chelsea bao lake la pili huku Torres akifunga la tatu naye Branislav Ivanovic kuifungia Chelea bao lake la nne.

Kocha wa Chelsea Roberto Di Matteo amefurahishwa na matokeo hayo, ambayo sasa yameiweka klabu hiyo kileleni mwa ligi hiyo kwa mara ya kwanza tangu Novemba mwaka wa 2010.

Chelsea sasa ina pointi sita baada ya mechi mbili nayo Reading imo katika nafasi ya 12 ikiwa na alama moja.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.