Jeshi la Syria laanza Mashambulio zaidi

Imebadilishwa: 23 Agosti, 2012 - Saa 15:52 GMT
Mwanjeshi wa Syria

Mwanjeshi wa Syria

Jeshi la Syria likisaidiwa na helikopta za kijeshi limeanzisha upya shambulio lake kwenye kiunga cha mji mkuu Damascus katika juhudi ya kufyeka uasi ulioko huko.

Upinzani unasema kuwa watu arobaini waliuawa mjini Damascus hapo jana na taarifa za hivi karibuni zinasema kuwa askari hao wameingia kitongoji cha Daraya.

Duru za upinzani zinasema kuwa askari wa vikosi vya serikali wamefanya msako wa nyumba kwa nyumba katika kitongoji kilicho kusini mwa mji cha Daraya baada ya mashambulio makali ya saa 24.

Imearifiwa kuwa hawakukabiliwa na upinzani wowote wakati wa msako huo kutoka kwa waasi ambao wanaonekana waliondoka katika eneo hilo katika kile kinachoaminika kuwa mchezo wa paka na panya.

Katika siku za hivi karibuni utawala umezidisha mashambulio yake pembezoni mwa Damascus, baada ya kung'olewa huko na waasi waliotangaza ushindi katika mji mkuu.

Wanaharakati wanasema kuwa ghasia hizi zimesababisha vifo vya raia wengi na mamia kuachwa bila makaazi.

Mapigano yameendelea huko Aleppo, ambako shirika la Amnesty linasema kuwa raia wanakabiliwa na ghasia za kuchukiza siku hadi siku. Jeshi la serikali linatumia mizinga na silaha nzito kwa mashambulio yasiyobainisha adui na mwananchi wa kawaida.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.