Tutu kuongoza Wakfu wa David Astor

Imebadilishwa: 23 Agosti, 2012 - Saa 16:37 GMT
Desmond Tutu

Desmond Tutu

Askofu mstaafu wa Afrika Kusini, Desmond Tutu, ambaye pia ni mwanaharakati mkongwe wa vita dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi nchini na mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, ameteuliwa kuwa mlezi mpya wa wakfu wa David Astor wakfu ambao huwatuza waandishi wa habari waliotia fora katika fani mbali mbali ya uandishi.

Tangazo hilo limetolewa huku wakfu huo, ukiadhimisha miaka mitano tangu ilipobuniwa kwa nia ya kuimarisha viwango vya uandishi wa habari barani Afrika.

Mwenyekiti wa wakfu huo David Burke, amesema ni heshima kubwa kwa wakfu huo na waandishi wote wa habari barani Afrika kuungwa mkono na kiongozi wa hadhi kama ya Askofu huyo, ambaye sifa zake zimeenekea kote duniani.

''uongozi wa Askofu tutu utaipa wakfu huo motisha hasa waandishi wachanga wa habari ambao wanashiriki katika miradi mbali mbali ya shirika letu'' alisema Bwana Burke.

Askofu Tutu ambaye ni askofu wa kwanza mweusi wa jimbo wa Cape Town, nchini Afrika Kusini, alikuwa mkosoaji mkubwa wa utawala wa ubaguzi wa rangi na alihudumu kama mwenyekiti wa tume ya haki na maridhiano nchini humo baada ya tume hiyo kuporomoka.

Tangu mwaka wa 2007, Askofu Tutu amekuwa mwenyekiti wa jopo la wazee ambao wanashirikiana kukuza amani na utengamano.

Wakfu wa David Astor ni shirika lililo na makao yake nchini Uingereza na linahusika na mikakati ya kuimarisha taalum ya uandishi wa habari kwa kuwapa misaada na mafunzo waandishi wa habari wachanga ili wakuze vipaji vyao.

Shirika hilo hutoa tuzo tatu kila mwaka kwa waandishi wa habari wanaohudumu nchini Kenya, Uganda na Tanzania.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.