Risasi zafyatuliwa katikati ya New York

Imebadilishwa: 24 Agosti, 2012 - Saa 16:52 GMT

Watu kadha wamepigwa risasi nje ya jengo maarufu la skyscraper mjini New York, Empire State Building, ambalo linavutia watalii.

Empire State Building mjini New York

Inavofahamika ni kuwa mwanamme mmoja alifyatua risasi naye mwenyewe alipigwa risasi na kuuliwa na polisi.

Meya wa New York, Michael Blomberg, alisema baadhi ya wale waliojeruhiwa pengine walipigwa risasi za polisi, lakini alisema majeruhi siyo mahtuti.

Mshambuliaji huyo ametajwa kuwa John Jeffrey Johnson - mpambi wa maduka ya nguo, ambaye alitolewa kazini mwaka jana.

Mtu aliyemuuwa ni mfanyakazi mwenzake wa zamani.

Eneo hilo la misafara mingi ya magari katika mtaa wa Manhattan, limefungwa na magari hayaruhusiwi kupita.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.