Mfuasi wa Gbagbo akamatwa Ghana

Imebadilishwa: 25 Agosti, 2012 - Saa 15:37 GMT


Familia ya mfuasi mashuhuri wa rais wa zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo, inasema kuwa jamaa yao amekamatwa katika nchi ya jirani, yaani Ghana.

Kiongozi wa sasa wa Ivory Coast, Alassane Ouattara

Familia ya Justin Kone Katinan inasema kuwa alikamatwa na polisi wa Ghana alipowasili nchini humo kutoka Afrika Kusini.

Wakuu wa Ivory Coast wamemshutumu Bwana Katinan kwamba anashughulika na kuchafua utulivu wa Ivory Coast, na kutoa nje mamilioni ya dola za taifa.

Mwandishi wa BBC nchini Ivory Coast anasema kukamatwa kwa Bwana Katinan kunaonesha ushirikiano unaozidi wa Ghana, baada ya mashambulio ya karibuni ambayo yalidaiwa kufanywa na waIvory Coast wanaoishi Ghana.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.