Uingereza haitaingia ubalozi wa Ecuador

Imebadilishwa: 26 Agosti, 2012 - Saa 17:32 GMT

Rais wa Ecuador, Rafael Correa, anasema kuwa Uingereza imeacha kile alichosema ni tishio la kuingia kwenye ubalozi wa Ecuador mjini London kumkamata muasisi wa Wikileaks, Julian Assange.

Rais wa Ecuador, Rafael Correa

Wizara ya Mashauri ya Nchi za Nje ya Uingereza ilipeleka barua kwa ubalozi huo iliyokusudiwa kuruhusu mazungumzo kuhusu Bwana Assange kuanza tena, lakini Uingereza imekanusha kuwa ilitishia wakati wowote kuingia ubalozini.

Bwana Correa alisema kuwa sasa anaona ugomvi wa kidiplomasia baina ya nchi mbili hizo umekwisha.

Bwana Assange anatakiwa aende Sweden, ambako wakuu wanamsaka kutokana na tuhuma za ubakaji.

Amepata hifadhi ya kisiasa nchini Ecuador, lakini anaweza kukamatwa akitoka kwenye ubalozi wa Ecuador mjini London.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.