Nigeria yateta na Boka Haram kwa siri

Imebadilishwa: 27 Agosti, 2012 - Saa 12:02 GMT

Abubakar Shekau kiongozi wa Boko Haram

Serikali ya Nigeria imesema imeanza mazungumzo yasiyo rasmi na kundi la Boko Haram, kujaribu kumaliza mashambulizi kutoka kundi hilo la wapiganaji wa kiislamu wenye msimamo mkali.

Msemaji wa rais wa nchi hiyo amesema mazungumzo hayo yanafanywa kwa siri, bila kufafanua zaidi.

Hivi karibuni kundi hilo lilikataa kushiriki katika mazungumzo ya amani.

Boko Haram wanaotaka kuazishwa kwa taifa la kiislamu nchini Nigeria, wanashutumiwa kwa mauaji ya mamia ya watu katika makanisa na maeneo mengine.

''Mfumo wa mazungumzo kwa njia ya siri unatumiwa kuweza kufikia kiini hasa cha tatizo kuweza kuelewa ni nini hasa hasira za watu hawa, kitu gani hasa kinaweza kufanywa kutatua migogoro hii,'' msemaji wa rais Reuben Abati amesema.

Amesema hatua hii inafanyika ili kuweza kuhakikishia amani na utulivu nchini Nigeria na usalama wa watu na mali''.

Baadhi ya akina mama wakiwalilia ndugu zao waliouawa katika moja ya mashambulizi ya Boko Haram

Msemaji huyo ameongeza kuwa mazungumzo hayo yamekuwa yakiendelea kuwahusisha baadhi ya wanachama wa kundi hilo.

Kundi la Boko Haram jina ambalo maana yake ni elimu ya nchi za magharibi ni marufuku, linafahamika kuwa na makundi kadhaa.

Hii ni taarifa ya kwanza kabisa iliyo rasmi kutoka kwa serikali ya Nigeria kuthibitisha kufanya mazungumzo na kundi hilo, mwandishi wa BBC nchini Nigeria Tomi Oladipo anaripoti.

Jaribio la kwanza kabisa la mazungumzo ya amani lilivunjika katika hatua ya awali kabisa.

Kundi hilo hadi sasa halijasema lolote kuhusu mazungumzo hayo ya kujaribu kufikia muafaka, mwandishi wetu anasema.

Nigeria imegawanyika kati ya eneo la kaskazini linalokaliwa na waislamu wengi zaidi na kisini kuliko na wakristo wengi zaidi.

Boko Haram wamekuwa wakifanya mashambulizi yake mengi maeneo ya kaskazini lakini pia baadhi ya maeneo mengine pia kama mji mkuu Abuja na katika jiji la Jos kuliko na uhasama mkubwa kati ya jamii ya waislamu na wakristo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.