shambulio la kutisha nchini Syria

Imebadilishwa: 28 Agosti, 2012 - Saa 15:16 GMT

Uharibifu uliosababishwa na shambulio hilo

Watu kumi na wawili wamefariki katika shambulio la bomu lililokuwa limetegwa ndani yagari, wakati wa mazishi katika mtaa wa Jaramana katika mji mkuu wa Syria, Damascus.

Shambulio hilo pia limesababisha majeruhi huku taarifa za vyombo vya serikali zikikadiria majeruhi hao kuwa 48.

Mazishi yaliyokuwa yanaendelea yalikuwa ya wafuasi wawili wa serikali ya rais Bashar al-Assad, kulingana na taarifa za chama kimoja cha upinzani nchini humo.

Wanaharakati wanakadiria idadi ya watu waliokufa katika ghasia za kisiasa nchini humo kuwa 20,000 . Wote hao wamefariki tangu mwezi Machi mwaka 2011,huku zaidi ya wengine milioni wakisemekana kutoroka nchi hiyo.

Wawili hao waliokuwa wanazikwa waliuawa katika shambulio la bomu mnamo siku ya Jumatatu.

Duru zinaarifu kuwa Texi moja ilitumiwa kulibeba bomu hilo kabla ya kulipuka.

Picha zilizotolewa baada ya shambulio lenyewe zilionyesha uharibifu mkubwa uliofanywa ikiwemo magari kuharibiwa pamoja na majengo yaliyokuwa yanazingira eneo hilo.

Ghasia ziliendelea kutokota kote nchini Syria hii leo ripoti zikielezea mashambulizi ya makombora katika mkoa wa Idlib, kaskazini mwa nchi.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.