Dunia imepuuza hali ya Mali

Imebadilishwa: 30 Agosti, 2012 - Saa 09:53 GMT

Hali ya njaa nchini Mali

Mjumbe maalum wa umoja wa mataifa wa haki za binadamu Valerie Amos amesema kuwa dunia imeshindwa kuwajibikia hali ya hatari kwa usalama wa raia wa Mali, ambako zaidi ya watu nusu milioni wametoroka makwao kutokana na vita.

Bi Valerie Amos, ambaye amekuwa akizuru kambi za wakimbizi ametoa wito wa msaada zaidi na ufadhili kuongezwa baada ya jamii ya kimtaifa kukusanya tu nusu ya pesa zinazohitajika kukabiliana na hali nchini humo.

Bi Amos yuko katika ziara ya siku tatu nchini Mali kujionea hali na athari za mzozo baada ya mapinduzi ya kijeshi mwezi Machi.

Tangu hapo, wapiganaji wa kiisilamu wa kabila la Tuareg wameteka maeneo ya kaskazini mwa Mali.

Mwandishi wa BBC David Loyn, ambaye yuko katika msafara wa Amos, anasema kuwa mzozo huo umeathiri pakubwa nchi hiyo na kufanya rasilimali kuwa dunia kabisa.

Juhudi za kutoa msaada katika eneo la kaskazini zimeathirika kutokana na mapigano.

Bei ya juu ya vyakula pamoja na kipato cha chini zimesababisha hali ngumu kwa wananchi wa Mali.

Serikali mpya ya muungano, iliundwa katika mji mkuu Bamako,mwishoni mwa wiki ikiahidi kuleta mageuzi na utahibiti katika maeneo ya kaskazini mwa nchi.

Wapatanishi kutoka muungano wa nchi za magharibi ECOWAS, wamefanya mazungumzo na wapiganaji hao, na hata kupeleka wanajeshi elfu tatu nchini Mali ikiwa ni sehemu juhudi za amani hazitazaa matunda.

Wapiganaji wa Tuareg waliteka eneo la kaskazini baada ya rais Amadou Toumani Toure kupinduliwa mwezi Machi.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.