''Marekani haikuhusika na mauaji ya mhubiri''

Imebadilishwa: 30 Agosti, 2012 - Saa 15:10 GMT

Vurugu Mombasa

Ubalozi wa Marekani mjini Nairobi umekanusha madai ya kuhusika na mauaji ya kiongozi mmoja wa kidini mjini Mombasa, Sheikh Aboud Rogo.

Wakili wa Rogo, Mbugua Mureithi na viongozi wengine wa Kiislamu wamedai kuwa Marekani ilihusika na mauaji ya kiongozi huyo wa kidini aliyepigwa risasi na watu wasiojulikana mjini Mombasa.

Kifo cha bwana Rogo kimesababisha machafuko na ghasia mjini humo na watu kadhaa wakiwemo maafisa wa polisi wamepoteza maisha yao.

Makanisa kadhaa yaliteketezwa na makundi ya vijana waliokuwa wakipinga mauaji hayo.

Lakini ubalozi huo umesema madai hayo hayana msingi wowote.

Hali imetulia mjini Mombasa baada ya usiku wa makabiliano mapya mjini humo kufuatia shambulizi la guruneti ambapo mtu mmoja aliuawa na wengine wengi kujeruhiwa.

Shambulio hilo limefuatia muda wa utulivu baada ya siku mbili ya makabiliano makali kati ya vijana waliofanya maandamano na polisi ambapo maafisa wanne wa polisi waliuawa.

Ghasia hizo zilisababishwa na kuuawa kwa mhubiri wa kiislamu Aboud Rogo Mohammed,aliyetuhumiwa na umoja wa mataifa pamoja na Marekani kuwa na uhusiano na makundi ya kigaidi

Mkuu wa polisi katika mkoa wa pwani ni Aggrey Adoli ameithibitishia BBC tukio hilo.

Polisi waelezea kuhusu mashambulizi

Polisi waelezea kuhusu mashambulizi

Sikilizamp3

Unahitaji toleo sahihi la Flash Player kucheza sauti/video

Cheza katika media player

Ripoti za mashambulizi ya hivi karibuni zingali zinatofautiana huku shirika la msalaba mwekundu likisema ni mtu mmoja tu aliyeuawa na wengine wawili kujeruhiwa vibaya katika shambulizi hilo la guruneti.

Baadhi ya vijana wanaozua vurugu walituhumu maafisa wa usalama kumuua marehemu Rogo wakisema kuwa alikuwa mwathirika wa mauaji ya kupangwa.

Hata hivyo, naibu msemaji wa polisi, Charles Owino alinukuliwa akisema kuwa kundi la wapiganaji la Alshabaab ndio walimuua mhubiri huyo katika kile alichosema ni jaribio la kupata kuungwa mkono zaidi na vijana.

Zaidi ya watu ishirini walikamatwa na polisi siku ya Jumanne kwa kuhusika na ghasia za siku ya Jumatano.

Wangali wamezuiliwa kesi yao ikitarajiwa kusikilizwa baadaye.

Baraza la usalama la umoja wa mataifa lilikuwa limemwekea vikwazo vya usafiri marehemu Rogo pamoja na kupiga tanji mali zake mwezi Julai , wakisema kuwa alitoa msaada wa kifedha kwa kundi la wapiganaji la Alshabaab

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.