Syria yahami chuo cha wanahewa

Imebadilishwa: 1 Septemba, 2012 - Saa 09:23 GMT

Serikali ya Syria inasema kuwa jeshi lake limeweza kuzuwia shambulio kubwa la wapiganaji dhidi ya chuo cha wanahewa karibu na mji wa Aleppo.

Shambulio lilofanywa Homs na ndege za wanahewa  wa  serikali yaSyria

Chuo hicho cha Rasm al-Abboud, ambacho kina kambi piya, ni moja kati ya kambi kadha za wanahewa zilizoshambuliwa katika siku za karibuni, huku wapiganaji wa upinzani wakijaribu kulingana na nguvu za serikali angani.

Helikopta na ndege za kijeshi zimetumika kusaidia wanajeshi wa serikali kwenye mapamabano.

Televisheni ya taifa imetangaza ushindi mwingi dhidi ya wale walioitwa magaidi wenye silaha, na waandishi wa habari wanasema jeshi la serikali linaonekana kuwa karibu kuudhibiti tena kikamilifu mji wa Aleppo au kukomboa na kudhibiti vitongoje vya mji mkuu, Damascus.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.