Balozi wa Algeria auwawa Mali

Imebadilishwa: 2 Septemba, 2012 - Saa 16:24 GMT
Wapiganaji wa Mali nje ya kituo chao cha polisi

Wakuu wa Algeria wanasema wanachunguza ripoti kuwa mwanabalozi mmoja wa Algeria ameuliwa na wapiganaji wa Kiislamu wa siasa kali nchini Mali.

Vuguvugu la Umoja na Jihadi Afrika Magharibi, ambalo linadhibiti karibu eneo lote la kaskazini mwa Mali, limetoa taarifa kwenye mtandao wa internet likisema kuwa limemuuwa mwanabalozi Tahar Touati.

Wanabalozi saba wa Algeria walitekwa nyara mwezi wa Aprili kutoka ofisi yao ya balozi mdogo kaskkazini mwa Mali.

Kundi hilo limeitaka serikali ya Algeria iwaachilie huru wapiganaji wa Kiislamu waliotekwa karibuni kusini mwa nchi, pamoja na kiongozi wa tawi la Al Qaeda kaskazini mwa Afrika.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.