Wachimba migodi wapumua kwa muda

Imebadilishwa: 2 Septemba, 2012 - Saa 13:49 GMT
Maandamano ya wachimba migodi wa Afrika Kusini

Nchini Afrika kusini upande wa mashtaka umefuta kwa muda mashtaka ya mauaji dhidi ya wachimba migodi 270 waliogoma.

Wachimba migodi hao walishtakiwa kwa mauaji ya wenzao 34 waliopigwa risasi na polisi mwezi uliopita wakati wa mgomo.

Wanasema kuwa wachimba migodi hao wataachiliwa huru katika wiki mbili zijazo.

Wananchi walishangzwa na uamuzi wa awali, wa kutumia sheria ya wakati wa ubaguzi wa rangi, kuwashtaki wachimba migodi kwa mauaji ya wenzao, ingawa risasi zote zilifyatuliwa na polisi.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.