Wengi wahudhuria mazishi ya Zenawi

Imebadilishwa: 2 Septemba, 2012 - Saa 09:34 GMT
Mazishi ya Meles Zenawi

Sifa na salamu zinatolewa juu ya waziri mkuu Meles Zenawi wa Ethiopia aliyeongoza kwa miaka mingi, ambaye anazikwa katika mji mkuu, Addis Ababa.

Viongozi wa Afrka na kwengineko wamekuwa wakionesha heshima zao pamoja na Rais Paul Kagame wa Rwanda, ambaye alisema Bwana Meles alitumia upeo wake mkubwa kuendeleza Afrika.

Maelfu ya wananchi wa Ethiopia - wengi wao wakiwa wamevaa T-shirt nyeusi zenye picha ya Bwana Meles - wamejaa kwenye medani kuu ya Addis Ababa.

Bwana Meles anasifiwa kuwa aliongoza maendeleo ya Ethiopia, lakini piya alilaumiwa kwa kukiuka haki za kibinaadamu.

Aliyechukua nafasi yake, Hailemaruiam Desalegn, ataongoza nchi hadi uchaguzi wa mwaka wa 2015.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.