Mjumbe maalum wa Syria ana kazi ngumu

Imebadilishwa: 3 Septemba, 2012 - Saa 08:35 GMT

Mjumbe Brahimi

Mjumbe mpya wa kimataifa katika mzozo wa Syria Lakhdar Brahimi, amelielezea jukumu lililo mbele yake kama ambalo huenda likamshinda.

Ameelezea hofu kuhusu uzito wa jukumu hilo.

Ameiambia BBC kuwa jamii ya kimataifa imezembea katika juhudi za kusitisha mauaji nchini Syria.

Mtangulizi wake , Kofi Annan, alijiuzulu mwezi Agosti baada ya mapigano kati ya majeshi ya serikali na waasi kuongezeka huku pande zote mbili zikipuuza mpango wa kusitisha mapigano aliopendekeza.

Bwana Brahimi, ambaye hutumika kwa majukumu ya mara kwa mara ya umoja wa mataifa kama mwanadiplomasia, aliteuliwa baada ya mtangulizi wake Kofi Annan, kujiuzulu akisema kuwa haoni njia ya kusuluhisha mzozo wa Syria na hivyo huenda asifaulu kutimiza jukumu lake.

Mapigano nchini Syria yamechacha licha ya juhudi za bwana Annan kujaribu kusitisha vita.

Wanaharakati wanasema kuwa takriban watu 20,000 wamefariki tangu mapambano kati ya serikali na waasi kuanza
mwezi Machi mwaka jana.

Mnamo siku ya Jumapili, shirika la kutetea haki za binadamu ambalo linaunga mkono waasi , lilisema kuwa zaidi ya watu 5,000 waliuawa mwezi Agosti pekee.

Wadadisi wanasema kuwa kibarua alichonacho bwana Brahimi ni mojawapo ya kazi ngumu sana lakini kama mwanadiplomasia mwenye uzoefu mkubwa wengi wanahisi kuwa ataweza kutoa mwongozo wa kukabiliana na hali ya Syria.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.