Hali mbaya ya wafungwa magerezani Chad

Imebadilishwa: 10 Septemba, 2012 - Saa 09:55 GMT

Ramani ya Chad

Wafungwa nchini Chad wanawekwa katika mazingira mabaya kiasi kuwa wanaotumikia kifungo wako katika hatari ya kufa jela.

Kulingana na shirika la Amnesty International, wafungwa wanawekwa katika magereza yaliyosongamana watu na kukosa hewa safi. Na yote hayo waliyashuhudia wakati walipotembelea magereza sita.

Ripoti ya shirika hilo imeelezea kisa kimoja ambapo wafungwa tisa walikufa gerezani baada ya kukosa hewa huku wengine saba wakiuawa kwa kupigwa risasi na walinzi.

Shirika hilo linasema kuwa wafungwa wanawake wanaishi katika hatari ya ubakaji na wengi wakiishi na watoto wao wenye hata miezi saba ndani ya magereza.

''Sio vyema wafungwa kuishi katika mazingira mabaya kama yale, mabaya sana kiasi cha mfungwa kuwa katika hatari ya kufia gerezani.'' alisema mtafiti mkuu wa shirika hilo Christian Mukosa.

"wafungwa wengi walikuwa na utapia mlo wakionekana wadhaifu sana. Baadhi walifungwa minyororo siku nzima wengi wakiugua maradhi ya ngozi, maradhi ya ngono, Malaria au Kifua kikuu" aliongeza Christian.

Shirika hilo limetoa wito kwa serikali kuchunguza madai hayo ya ukiukwaji wa haki za binadamu. Serikali ya Chad bado haijajibu ripoti hiyo ya Amnesty.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.