Marekani adui mkubwa wa Pakistan

Imebadilishwa: 11 Septemba, 2012 - Saa 07:09 GMT

Daktari aliyesaidia majasusi wa Marekani kupata maficho ya Osama bin Laden ameambia televisheini ya Marekani kuwa shirika la ujasusi la nchini humo, ISI, linaiona Marekani kama adui wake mkubwa zaidi.

Kwenye mahojiano kutoka chumba chake gerezani mjini Peshawar, Daktari Shakil Afridi, aliambia kituo cha Fox News kuwa maafisa wa shirika hilo waliomhoji walimwambia kuwa alisaida adui mkubwa wa Pakistan , adui mbaya hata kuliko India.

Kuhusu serikali ya Pakistan, Daktari, Afridi, alitoa taswira ya kile alichokiita utawala wa mateso ya watu magerezani.

Aliongeza kuwa wafungwa wenzake walimwambia kuwa walishauriwa watumie mbinu za uongo ili wasiweze kuhojiwa na majajusi wa CIA walio nchini humo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.