Muingereza akamatwa Uganda kwa Ushoga

Imebadilishwa: 14 Septemba, 2012 - Saa 15:52 GMT

Msanii moja toka Uingereza amekamatwa nchini Uganda kwa madia ya kuandaa na kuonyesha mchezo wa kuigiza kuhusu ushoga.

David Cecil katika mahakama ya Makindye

Polisi wanasema kuwa Muingereza huyo alionyesha mchezo huo wa kuigiza licha ya kwamba Uganda ilipiga marufuku kwa muda onyesho hilo.

Mtayarishi David Cecil wa Uingereza alifikishwa katika mahakama moja mjini Kampala na kushitakiwa kwa madia ya kukaidi na kupuuza amri ya serikali.

Mahakama hiyo iliambiwa kuwa Bwana Cecil alionyesha mchezo huo kwa jina "The river and the mountain" katika ukumbi wa Tilapia Cultural Center taraehe 17 Agosti na pia katika ukumbi mwengine wa Mish Mash Cultural Center tarehe 26 Agosti mjini Kampala.

Mahakama hiyo ya Kampala ilikataa kuamuachilia Muingereza huyo kwa dhamana na badala yake kuagiza awekwe katika gereza la Luzira hadi siku ya jumatatu ,Septemba 17 ambapo kesi yake inatarajiwa kuendelea.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.