Wachimba migodi wakataa pendekezo la mishahara

Imebadilishwa: 14 Septemba, 2012 - Saa 11:54 GMT

Wachimba Migodi

Wafanyakazi wa migodini nchini Afrika Kusini wamekataa pendekezo lililotolewa la kiwango cha mishahara ambacho wanaweza kuongezwa.

Hatua hii imeondoa matumaini ya kumalizika kwa migomo ya wachimba migodi ambayo imekuwa ikiendelea kwa wiki tatu sasa.

Wachimba migodi hao, walisema kuwa kiwango hicho ni cha chini sana ikilinganishwa na matakwa yao ya dola elfu moja miatano.

Migomo hiyo imekumbwa na machafuko ikiwemo mauaji ya wachimba migodi 34 waliouawa na polisi.

Kadhalika migomo ilisambaa hadi katika migodi mingine nchini Afrika Kusini nchi ambayo inauza nje madini mengi .

Uzalishaji wa madini umeathirika sana tangu migodi kufungwa.

Wachimba migodi hao walikataa pendekezo la kampuni ya madini ya Lonmin katika mkutano wao waliouandaa karibu na mgodi huo siku ya Ijumaa.

Wanasema kuwa kulingana na pendekezo hilo, wanaongezwa tu randi elfu moja pesa za Afrika Kusini kila mwezi ambazo ni kidogo sana.

Wachimba migodi hupata kati ya randi elfu nne na elfu tano.

Viongozi wa migomo wametishia kuitisha mgomo wa kitaifa ikiwa matakwa yao hayatatimizwa.

Wachimba migodi hao wanaungwa mkono na chama cha wafanyakazi chenye msimamo mkali pamoja na kile cha sekta ya ujenzi.

Chama cha kitaifa cha wachimba migodi, ambacho kina ushirikiano na chama cha ANC,kiliambia BBC kuwa kina wasiwasi kuhusu visa vya ghasia na visa vingi vya watu kupoteza kazi zao katika sekta madini.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.