Syria imekiuka haki za binadamu

Imebadilishwa: 17 Septemba, 2012 - Saa 10:51 GMT

Kikao cha Umoja wa mataifa kuhusu Syria

Tume ya Umoja wa mataifa inayochunguza ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Syria, imekusanya majina ya washukiwa vitendo vya uhalifu wa kivita nchini humo.

Wachunguzi wa tume hiyo wanawashutumu wanajeshi wa serikali kwa kuhusika katika uhalifu wa kivita.

Ripoti hiyo ni mojawapo ya ripoti zinazoikosoa zaidi serikali ya Syria kuwahi kupokelewa na Umoja wa Mataifa.

Mkuu wa tume hiyo Paulo Pinheiro, alisema kuwa lina ushahidi wa kutosha kuhusiana na madai hayo.

Alisema kuwa ana orodha ya majina ya washukiwa wakuu wa uhalifu wa kivita na kutaka Umoja wa mataifa kuwasilisha kesi ya uhalifu wa kivita dhidi ya Syria kwa Umoja wa Mataifa.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-Moon ametoa wito kwa baraza hilo la haki za binamu kuchukua hatua.

Wakati huohuo, shirika la kutetea haki za kibinadamu la Huma Rights Watch, limesema kuwa lina ushahidi wa kuthibitisha kuwa waasi nchini syria wamewatesa mateka mbali na kuwauwa wengine.

Shirika hilo ilikusanya ushahidi mwezi jana wa mauaji na mateso dhidi ya mateka yanayotekelezwa na upinzani katika mji wa Allepo na maeneo jirani .

Ripoti ya shirika hilo inalenga madai ya mauaji ya watu wanne wa familia moja na vuguvugu la Free Syrian Army.

Human Rights Watch linasema kasi ambapo watu hao waliuwawa inafanya madai ya upinzani kuwa walitendewa haki kuwa urongo mtupu.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.