Boko Haram wamuua mwanasheria mkuu

Imebadilishwa: 18 Septemba, 2012 - Saa 15:54 GMT

Maafisa wa utawala nchini Nigeria wanasema kuwa watu wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi la Boko Haram wamemuua mwanasheria mkuu wa jimbo la Borno Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, Zanna Malam Gana.

Watu waliokuwa wamejihami, pia walimpiga risasi na kumuua aliyekuwa mkuu wa magereza Ibrahim Jarmam katika jimbo jirani la Bauchi.

Mnamo siku ya Jumatatu, polisi walithibitisha kumuua afisaa mkuu wa kundi hilo ambaye anaaminika kuwa msemaji mkuu.

Kundi la Boko Haram limethibitisha kufanya mauaji ya mara kwa mara Kaskazini mwa nchi ambapo mamia ya watu wameuawa.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.