Migawanyiko ya ANC Afrika Kusini

Imebadilishwa: 19 Septemba, 2012 - Saa 11:35 GMT

Maandamano ya Cosatu

Migawanyiko mikubwa imezuka katika muungano kati ya chama tawala nchini Afrika Kusini ANC na washirika wake katika muungano wa vyama vya wafanyakazi COSATU.

Ripoti ya kisiasa iliyotayarishwa na uongozi wa muungano huo inayoangazia utumiaji wa vikundi vya kutekeleza mauaji kuwaangamiza wapinzani wa kisiasa, vimeshutumiwa vikali .

Wakati raia wa Afrika Kusini wakisherehekea kumalizika kwa mgomo usio rasmi wa wiki tano katika mgodi ulio wa tatu kwa ukubwa duniani wa uchimbaji madini ya Platinum, viongozi wa muungano wa wafanyakazi walikuwa katika mjadala mkubwa.

Miungano hiyo ilifahamu kwamba washiria wake walihusika katika mgomo wa Marikana ulioshuhudia umwagikaji damu na kusababisha vifo vya wachimba mgodi 45 wengi ambao waliuawa na polisi.

Ripoti hiyo ya kisiasa iliyowasilishwa katika mkutano wa miungano hiyo ya wafanyakazi ilijumusha shutuma kali kwa kile kilichotajwa kuwa kukithiri kwa rushwa ambayo sasa inaathiri sekta zote za serikali.

Miungano hiyo imeangazia pia kile inachotaja kuwa mauaji yanayotokea sasa ndani ya vuguvugu wakati watu wanajaribu kutumia ushawishi wa kisiasa kujipatia mali.

Ripoti hiyo imewataja wanachama cha ANC na wa miungano ya wafanyakazi waliouawa katika miaka ya hivi karibuni kutokana na kuzuka kwa makundi hayo ya kutekeleza mauaji katika majimbo tofauti dhidi ya watu wanaopinga rushwa.

Akiijibu ripoti hiyo katibu mkuu wa ANC, Gwede Mantashe amesema hilo ni jaribio la kuitenganisha miungano kutoka kwa chama hicho. Lakini huku maandamano Afrika Kusini yakiwa ni tukio la karibu kila siku, rais Zuma na washirika wake katika miungano hiyo wanajaribu kuidhibiti hali hiyo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.