Wakristo wakopti kukamatwa Marekani

Imebadilishwa: 19 Septemba, 2012 - Saa 11:15 GMT

Maafisa wa utawala mjini Cairo, wameamuru kukamatwa kwa wakiristu saba wa kikopti raia wa Misri wanaosihi nchini Marekani kwa kuhusika na utengezaji wa filamu iliyozua ghadhabu miongoni mwa waisilamu wengi kote duniani.

Filamu hiyo ambayo inamkejeli mtume Muhammad ilizua ghasia na kero katika mataifa ya kiisilamu kwa namna ilivyomdhihaki Mtume.

Hata hivyo haijabainika mtunzi wa filamu hiyo lakini imehusishwa na wakristo wa kikopti wanaoishi nchini Marekani.

Kibali cha kumkamata mchungaji Terry Jones nchini Marekani kimetolewa.

Mwanamke mmoja na wanaume saba akiwemo Jones, wanatuhumiwa kwa kuitusi dini ya kiisilamu na kuchochea ghasia za kidini , kwa mujibu wa taarifa za mwendesha mkuu wa mashtaka.

Taarifa hiyo ilisema kuwa shirika la polisi wa kimataifa la Interpol, watafahamishwa kuhusu vibali hivyo.

Ombi pia litatolewa kwa maafisa wa kisheria nchini Marekani. Inaarifiwa kuwa ikiwa wote waliotuhumiwa watapatikana na hatia huenda wakahukumiwa kifo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.