Wachimba migodi warejea kazini

Imebadilishwa: 20 Septemba, 2012 - Saa 09:10 GMT

Wachimbaji wa Marikana


Wachimba migodi nchini Afrika Kusini wameanza kurejea kazini katika mgodi wa madini ya Platinum wa Marikana

Mgodi huo ulikuwa kitovu cha ghasia na mauaji ya wachimba migodi 44 waliozua ghasia wakati wakigoma kwa wiki sita kudai nyongeza ya mishahara .

Mapema wiki hii wachimba migodi waliafikia makubaliano ya asilimia 22 ya nyongeza ya mishahara ndipo wakakubali kurejea kazini.

Wamiliki wa mgodi wa Lonmin ambao ni wa tatu kwa ukubwa katika kuzalisha madini ya Platinum duniani, walielezea kupata hasara kubwa ya kifedha wakati mgodi huo ulipofungwa kufuatia mgomo wa wachimba migodi.

Jopo maalum limeundwa nchini humo kuchunguza vifo vya wachimba migodi waliouawa na polisi wakati wa migomo hiyo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.