Watu wa Benghazi wataka amani

Imebadilishwa: 22 Septemba, 2012 - Saa 09:38 GMT

Maelfu ya Walibya wamefanya mhadhara katika mji wa Benghazi, mashariki mwa Libya, kuunga mkono demokrasi na kuwapinga wapiganaji wa Kiislamu.

Maandamano ya kupinga wapiganaji mjini Benghazi

Waandamanaji waliisihi serikali ya Libya iyapige marufuku makundi ya wapiganaji ambao wamekataa kukabidhi silaha zao tangu vita dhidi ya Kanali Gaddafi mwaka jana.

Waandamanaji wanataka serikali izidishe jeshi na polisi, na walimsifu balozi wa Marekani aliyeuliwa mjini humo juma lilopita.

Waliimba wakati wakiandamana kuelekea medani kuu ya Benghazi.

Muandamanaji mmoja, Faisla al-Naas, alieleza sababu zao:

"Sisi tunaandamana kupinga kundi lenye silaha ambalo halidhibitiwi na serikali.

Wapiganaji hawa wanafaa kujiunga na serikali ili watu wakae kwa salama.

Nchi yetu imekuwa na mtafaruku."

Maandamano mengine ya kuunga mkono wapiganaji yalikuwa madogo sana.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.