Al Shabaab yamegeka baadhi wakijiondoa

Imebadilishwa: 24 Septemba, 2012 - Saa 12:42 GMT

Al Shabaab

Kundi moja la wapiganaji wa Al Shabaab, nchini Somalia, limesema linajiondoa kwenye kundizoma la wapiganaji hao.

Chama cha Hizbul Islam kimeiambia BBC kwamba kuanzia leo hakitakuwa na uhusiano wowote na Al Shabaab.

Kuna dalili kwamba kundi hilo sasa huenda likaingia katika majadiliano na serikali ya Somalia.

Mwandishi wa idhaa ya kisomali ya BBC amesema mgawanyiko huo katika kundi hilo ni hatua muhimu.

Al Shabaab lenye itikadi kali za dini ya kiislamu liliondolewa katika mji mkuu Mogadishu mwaka uliopita na limekuwa likishindwa nguvu katika makabliano na vikosi vya Umoja wa Afrika, AMISOM.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.