Sudan na Sudan Kusini zarejea mezani

Imebadilishwa: 24 Septemba, 2012 - Saa 16:27 GMT

Mkutano wa Sudan na Sudan Kusini Ethiopia

Marais wa Sudan na Sudan Kusini wameendelea na mazungumzo yao hii leo kuhusu mgogoro ambao ulisababisha mapigano mapema mwaka huu.

Mambo muhimu katika mkutano huo unaofanyika Ethiopia ni pamoja na usalama wa mpaka, kuchangia mapato ya mafuta na eneo lililozusha mzozo la Abyei mwezi April, chini ya mwaka mmoja baada ya Sudan Kusini kujitenga.

Mkutano huo unakusudia kupata makubaliano jadidi kuhusu masuala ya mafuta na mipaka.

Baada ya masaa mawili ya mazungumzo siku ya Jumapili,msemaji wa serikali ya Sudan, Badr El-Din Abdallah, alisema kuwa hatua zimepigwa kati ya pande zote mbili lakini swala la amani ndilo bado linazua utata

Umoja wa mataifa umetishia kuziwekea pande zote mbili vikwazo ikiwa hazitaafikia makubaliano na amani ya kudumu

Sudan Kusini ilijipatia uhuru mwaka jana kutoka kwa Sudan baada ya makubaliano ya amani kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya zaidi ya miaka kumi.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.