Baraza la Umoja wa Mataifa laanza vikao

Imebadilishwa: 25 Septemba, 2012 - Saa 16:09 GMT

Rais wa Marekani Barack Obama

Baraza la umoja wa mataifa limefungua rasmi mkutano wake mjini New York.

Rais Barack Obama amefungua mkutano huo kwa hotuba ya kumsifu balozi wa zamani wa Libya ambaye aliuawa katika shambulizi dhidi ya ubalozi wa Marekani mjini Benghazi mapema mwezi huu.

Alisema kuwa Marekani haitachoka katika juhudi zake kuwasaka wauaji wa balozi huyo na kuwawajibisha kisheria.

Alilaani ghasia hizo zilizotokea kufuatia ghadhabu katika nchi za kiisilamu baada ya kutolewa kwa filamu iliyokejeli Mtume Muhammad na dini ya kiisilamu.

Obama amelaani filamu hiyo na kusema Marekani haina uhusiano wowote na filamu hiyo na vile vile amelaani waliotengeza filamu hiyo.

Rais Obama ameitaka serikali ya rais wa Syria Bashar Assad kuondoka mamlakani na kuwa Marekani itafanya kila iwezalo kuzuia Iran kuwa na zana za nuklia.

Katika hotuba yake ya ufunguzi, naye katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon, alikitaja kipindi hiki kama kipindi cha msukosuko ,mpito na mageuzi.

Alionya kuwa fursa inaweza kuwa inatoweka ya kupata suluhu baina ya Israil na Wapalestina, ya kuwa na mataifa mawili.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.