Gazeti la Misri lajibu vibonzo Ufaransa

Imebadilishwa: 26 Septemba, 2012 - Saa 10:14 GMT

Katika picha nyingine wanaume wawili waarabu wanaonekana mmoja kando ya mwingine

Gazeti moja nchini Misri limeanzisha kampeini ya kulipiza kisasi dhidi ya jarida la nchini Ufaransa la Charlie Hebdo lililochapisha picha za kumkejeli Mtume Muhammad .

Al-Watan, gazeti la kila siku lilichapisha vibonzo kumi na tatu vyenye maada "Fight cartoons with cartoons" yaani tumia vibonzo kupigana na vibonzo.

Moja ya vibonzo hivyo inaonyesha miwani na kwa mbali jumba la World Trade Center likichomeka , kichwa cha kibonzo hicho kikisoma "Western glasses for the Islamic world", yaani taswira ya nchi za Magharibi kuhusu dunia ya kiisilamu.

Vibonzo vilivyochorwa na gazeti la Charlie Hebdo, vilikuwa vya kuwafanyia mzaha waisilamu walioandamana kupinga filamu ya Marekani iliyokejeli Mtume Muhammad na dini ya kiisilamu.

Takriban watu 50 waliuawa katika maandamano yaliyokumbwa na ghasia wiki mbili zilizopita katika nchi za kiisilamu.

Kurasa mbili za Al-Watan kuhusu vibonzo hivyo ni sehemu ya makala ya kurasa kumi na mbili yaliyokuwa jibu la gazeti hilo kwa gazeti la Charlie Hebdo.

Makala hayo pia yalijuimsha tathmini za wachoraji vibonzo mashuhuri kutoka Mashariki ya kati kama vile Amr Hamzawi na wasomi kama Mufti wa Misri, Ali Gomaa.

Moja ya vibonzo hivyo ilionyesha mwanaume mzungu akimkemea mzee mmoja mwenye ndevu huku akimuita gaidi hadi anapoona kuwa ni muisraeli na kisha kumpa mauwa.

Wasomaji wa gazeti hilo walifurahi sana kuona makala hayo ambayo ndiyo jibu la gezti hilo kwa lile la Ufaransa. Gazeti hilo hukosoa vikali chama cha Muslim Brotehrhood chake rais Mohammed Morsi

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.