E.Guinea yataka Ufaransa ikomeshe uchunguzi

Imebadilishwa: 26 Septemba, 2012 - Saa 17:01 GMT

Teodorin Nguema Obiang Mangue

Equatorial Guinea imeitaka mahakama ya kimataifa ya haki ICJ, kuamuru Ufaransa kusitisha uchunguzi wa tuhuma za ufisadi dhidi ya familia inayotawala nchi hiyo.

Mahakama hiyo imethibitisha ombi la Equatorial Guinea, lakini ikasema kuwa lazima Ufaransa mwanzo itambue mahakama hiyo

Mwezi Julai, Ufaransa ilitoa kibali cha kumkamata mwanawe rais wa nchi hiyo kwa tuhuma za ubini wa pesa.

Pia ilipiga tanji nyumba ya kifahari ya Teodorin Nguema Obiang Mangue mjini Paris.

Hata hivyo bwana Obiang amekana kufanya makosa yoyote.

Taarifa ya wakili wa serikali ya Equatorial Guinea kwa mahakama ya ICJ, ilisema kuwa hatua ya Ufaransa inakiuka misingi ya usawa baina ya nchi , uhuru na heshima ya familia hiyo kuwa na kinga dhidi ya kushtakiwa kwa makosa ya jinai.

Lakini mahakama hiyo imesema kuwa hakuna hatua yoyote itachukuliwa hadi Ufaransa itambue uwezo wa mahakama ya ICJ kusikiliza kesi hiyo.

Maafisa wa Ufaransa bado hawajatoa tamko lolote kuhusu hatua ya Equatorial Guinea

Majaji wa Ufaransa, wanachunguza madai ya tuhuma za uporaji wa pesa za umma dhidi ya rais wa nchi hiyo President Teodoro Obiang Nguema Mbasogo na mwanawe Teodorin,ambaye sasa ni makamu wa rais na kununua mali nchini Ufaransa kwa kutumia pesa hizo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.