Maelfu waomboleza kifo cha Omran Ben Shaaban

Imebadilishwa: 26 Septemba, 2012 - Saa 11:06 GMT

Jeneza la Omran ben Shaaban

Zaidi ya watu 10,000 nchini Libya walikusanyika kuomboleza kifo cha mmoja wa waasi waliosifika kwa kumkamata hayati
Muammar Gaddafi mwaka jana.

Omran Ben Shaaban alifariki Jumanne iliyopita baada ya kutekwa , kupigwa risasi na kuteswa na wafuasi wa hayati Gaddafi.

Mwili wa kijana huyo aliyekuwa na miaka umri wa miaka 22, ulipelekwa nyumbani kwao mjini Misrata kwa mazishi.

Serikali ilisema kuwa itampa mazishi ya kishujaa kijana huyo huku kukiwa na wito wa serikali kulipiza mauaji yake.

Shaaban alikamatwa na watu waliokuwa wamejihami mnamo mwezi Julai, na kuzuiliwa kwa siku 50 mjini Bani Walid, iliyokuwa ngome ya Gaddafi Kusini Mashariki mwa Tripoli.

Aliachiliwa wiki jana baada ya juhudi za upatanishi kufanywa na kiongozi wa mpito wa nchi hiyo Mohammed Magarief.

Bwana Shaaban aliwasili mjini Misrata akiwa na alama za mateso pamoja na alama ya risasi kwenye uti wake wa mgongo. Alipelekwa mjini , Paris kwa matibabu ingawa alifariki baadaye.

Shaaban alianza kujulikana tarehe 20 mwezi Oktoba mwaka jjana, wakati alipoonekana katika sehemu alikokamatwa marehemu kanali Gaddafi mjini Sirte.

Wengi wameomboleza kifo cha Shaaban, aliyetambulika kama shujaa huku serikali ikisema itafanya juhudi za kuwasaka watesi wa Shaaban na kuwahukumu.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.