Mbunge kizimbani kwa matamshi ya uchochezi

Imebadilishwa: 27 Septemba, 2012 - Saa 17:38 GMT

Wamaasai wakitaka Bwana Ferdinand Waititu kufutwa kazi

Mahakama nchini Kenya imemweka rumande Waziri msaidizi wa maji Ferdinand Waititu anayetuhumiwa kutoa matamshi ya uchochezi.

Hata hivyo, Waititu aliyejisalimisha Mahakamani na wakili wake baada ya kuwakwepa Polisi tangu Jumanne iliyopita, hakutakiwa kujibu mashtaka.

Waziri huyo ambaye pia ni mbunge wa eneo la Embakasi alionyeshwa kwenye Mtandao wa Yu-Tube akikashifu kabila la Wamaasai katika eneo bunge lake ambako kuna idadi kubwa ya watu kutoka jamii ya wakikuyu.

Bwana Ferdinand alifikishwa mahakamani akiwa amefungwa pingu na kushtakiwa kwa kutoa maneno ya chuki dhidi ya jamii ya wa-maasai.

Mwanasiasa huyo wa Kenya ameshtakiwa kufuatia amri ya Mkuu wa Mashtaka aliyetaka akamatwe na kuwajibishwa kisheria kutokana na matamisi yake ya kichochezi.

Ni waziri wa pili kufikishwa mahakamani kwa matamshi ya uchochezi wa kikabila mwezi huu.

Kuna wasiwai kwamba wanasiasa wanatumia matamashi ya uchochezi kuleta uhasama kati ya jamii mbali mbali wakati uchaguzi mkuu ukitarajiwa mwezi Machi mwaka ujao.

Ghasia na vurugu kati ya jamii hasimu nchini Kenya imesababisha mauaji ya watu miamoja Kusini Mashariki mwa Kenya katika eneo la Tana River.

Ili kuweza kuzuia kutokea tena kwa ghasia zilizokumba Kenya baada ya uchaguzi mwaka 2007 katiba mpya iliyopitishwa miaka miwili iliyopita,inasema kuwa waziri yeyote anayeshtakiwa kwa kosa la kuchochea uhasama kati ya makabila tofauti hatagombea wadhifa wowote wa kisiasa ila tu ikiwa kesi yake itatupiliwa mbali na mahakama.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.