11 Wauwa wakila kiapo nchini Kenya

Imebadilishwa: 27 Septemba, 2012 - Saa 18:16 GMT

Wanachama wa MRC

Watu 11 wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi haramu la Mombasa Republican Council (MRC) wameuwawa katika eneo la msitu wa Bamba eneo la Kilifi katika Mkoa wa Pwani.

Mkuu wa Polisi eneo la Pwani ya Kenya Bwana Aggry Adoli amethibitisha tukio hilo akisema kuwa wanakijiji waliwaona watu walioshukiwa kuwa wanachama wa MRC wakiingia msituni na kuwafuata na kisha kuwaua baadhi ya watu waliokuwa kwenye kundi hilo.

Duru zinasema kuwa watu hao walikuwa miongoni mwa watu walioshukiwa kuwa majambazi.

Walikamatwa na silaha za kijadi kama vile panga na visu. Polisi wanasema kuwa mmoja wao alikuwa mganga wa kienyeji

Eneo la Pwani mwa Kenya limekuwa na migogoro ya kila aina kuanzia kwa uhasama kati ya jamii hasimu zinazoishi pembezoni mwa mkoa huo.

Polisi wamekua wakilaumiwa kwa kukosa kudhibiti ulinzi mkoani humo hasa wakati huu wa heka heka za maandalIzi ya uchaguzi utakaofanyika mwezi Machi mwaka ujao.

Hata hivyo bwana Adoli anasema kuwa utovu wa usalama sio kosa la polisi bali ni kutokana na matatizo yanayokumba jamii za eneo hilo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.