Mapigano makali mjini Alepo

Imebadilishwa: 28 Septemba, 2012 - Saa 15:45 GMT

Makabiliano mjini Alepo

Mapigano makali yameripotiwa kuzuka mjini Aleppo , mji wa pili kwa ukubwa nchini Syria.

Duru zinasema kuwa makabiliano yaliyoshuhudiwa ndiyo makali kabisa kutokea katika siku za hivi karibuni.

Waasi walianza mashambulizi mapya dhidi ya jeshi mnamo siku ya Alhamisi na kusema kuwa vita vya kuutwa mji wa Alepo ndiyo vimeanza.

Lakini ripoti zinasema kwamba waasi hao wametaabika katika kupiga hatua zozote muhimu dhidi ya jeshi la rais Assad.

Wanaharakati na wenyeji wa mji huo, wanasema kuwa, mapambano yameenea hadi katika maeneo yaliyokuwa hayana vurugu, na sasa yanawahusisha wanamgambo wa kikurdi kutoka kwa kundi linalotaka kujitenga la PKK, ambalo wanalishuku kuunga mkono wapiganaji wa Assad.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.