Waziri alaani ubakaji Tunisia

Imebadilishwa: 28 Septemba, 2012 - Saa 14:11 GMT

Wanawake wa Tunisia wakiandamana

Waziri wa wanawake nchini Tunisia, Sihem Badi,amelaani vikali kitendo cha polisi wawili kumbaka mwanamke ambaye baadaye yeye na mpenzi wake walishtakiwa kwa kosa la utovu wa nidhamu hadharani.

Bi Badi ametoa wito wa kushtakiwa kwa polisi hao akisema kuwa hakuna mtu ana kinga ya kukabiliwa na sheria.

Msemaji wa serikali (Samir Dilou) alisema kuwa serikali iko tayari kupambana na dhulma za aina yote dhidi ya wanawake, lakini haiwezi kuingilia uchunguzi unaoendelea kwa sababu ya uhuru wa mahakama za nchi hiyo.

Wakili wa mwathiriwa, alilalamika na kusema kuwa serikali inapaswa kulaumiwa kwa vitendo vya polisi kuwadhulumu wanawake, kwa sababu ya sheria zake dhaifu kuhusu dhulma dhidi ya wanawake.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.