Al-Shabaab waondoka Kismayo

Imebadilishwa: 29 Septemba, 2012 - Saa 12:08 GMT

Kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Somalia, Al Shabaab linasema kuwa limeondoka katika ngome yao kubwa iliyobaki, yaani mji wa Kismayo.

Kismayo

Wakaazi wa Kismayo waliiambia BBC kwamba wapiganaji hao waliondoka usiku na kwamba mji sasa ni shuwari.

Majeshi ya Kenya na serikali ya Somalia, ambao walikuwa wakipigana na Al Shebaab kilomita kadha nje ya mji hapo jana, bado hawakuingia mjini.

Kismayo ni bandari ya pili ya Somalia kwa ukubwa na ikileta pato muhimu kwa al-Shabaab.

Wakaazi wa Kismayo wanasema waliamka leo asubuhi na kukuta Al Shebaab wameshaondoka.

Kwenye ukurasa wao wa mtandao wa internet wa twitter, kundi la al-Shabaab limetoa tangazo hili: "jana usiku, baada ya miaka mitano, utawala wa Kiislamu mjini Kismayo ulifunga ofisi zake".

Wanajeshi wa Kenya na serikali ya Somalia bado hawakuingia ndani ya mji.

Msemaji wa jeshi la Kenya aliiambia BBC kwamba ana wasiwasi kuwa kuondoka kwa al-Shabaab pengine ni mtego.

Kwa hivo kwa sasa, Kismayo haidhibitiwi na mtu yoyote.

Yote yanategemea vipi serikali ya Somalia na washirika wao wa Umoja wa Afrika watavosarifu maslahi yao yanayogongana, kudhibiti mji huo wenye bandari na unaoleta pato.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.