Shule ya kanisa yashambuliwa Nairobi

Imebadilishwa: 30 Septemba, 2012 - Saa 13:26 GMT

Shambulio la guruneti la mkononi dhidi ya shule ya Jumapili ya watoto wa Kikristo mjini Nairobi limeuwa mtoto mmoja na kujeruhi wengine kadha.

Polisi wa Kenya

Mkuu wa polisi wa Nairobi, Moses Ombati, ameliambia gazeti la Daily Nation kwamba watu watatu wamekamatwa, na kwamba watu hao walionekana wakipiga picha za kanisa la Saint Polycarp lilolengwa.

Msikiti ulio karibu na hapo ulishambuliwa na vijana waliokuwa na hasira.

Afisa wa polisi wa Nairobi aliwasihi watu wawe watulivu.

Shambulio lilitokea katika mtaa wa Juja Road, unaopakana na mtaa wa Eastleaigh.

Inaaminiwa kuwa guruneti lilirushiwa kanisa la Saint Polycap kama saa tano punde baada ya misa ya asubuhi.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.