Maduka na ofisi zafungwa Kismayo

Imebadilishwa: 30 Septemba, 2012 - Saa 15:28 GMT


Wakaazi wa mji wenye bandari wa Kismayo, kusini mwa Somalia, wanasema bado mji huo haudhibitiwi na mtu yoyote.

Mapigano kuania Kismayo

Siku ya Ijumaa vikosi vya Kenya na serikali ya Somalia vilifika kaskazini ya mji huo na kupelekea wapiganaji wa Kiislamu wa al-Shabaab kuondoka.

Mizinga ilisikika usiku, lakini vikosi hivo bado viko nje ya mji.

Kuna taarifa kuwa wazee kadha wameuliwa na watu wenye silaha na shule na maduka karibu yote yamefungwa.

Kismayo ilikuwa ngome kubwa ya mwisho ya al-Shabaab, ambako wakiweza kuagiza silaha kutoka nchi za nje na kupokea pato kwa kuwatoza kodi wafanya-biashara.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.