Wasiwasi warudi Pibor, Sudan Kusini

Imebadilishwa: 30 Septemba, 2012 - Saa 15:59 GMT

Kuna mvutano na wiwasi katika mji wa Pibor, Sudan Kusini, karibu na mpaka wa Ethiopia.

Ghasia za Sudan Kusini zinatokea mara kwa mara

Shirika la kimataifa la msaada wa matibabu, MSF, limewaondosha wafanyakazi wake wa kigeni na wengi walio wenyeji wamekimbilia vichakani.

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa katika Sudan Kusini, Hilde Johnson, amesema hali katika mji wa Pibor ni ya wasiwasi, na kuna ripoti kuwa wakaazi wamekimbilia vichakani.

Kuondoshwa kwa wafanyakazi wa MSF kumewaacha watu kama 90,000 bila ya huduma za afya.

Tisho linatokana na kiongozi wa wapiganaji, David Yauyau, ambaye amewavutia vijana wa kabila la Murle.

Inaarifiwa kuwa wenyeji wamekerwa na wanajeshi wa serikali ya Sudan Kusini waliowekwa kwenye eneo hilo, wengi wao kutoka kabila la maadui wao la Nur.

Inasemekana wanajeshi hao wamewapiga na kuwabaka baadhi ya wenyeji.

Umoja wa Mataifa unasema unafuatilia hali hiyo kwa makini na uko tayari kutuma askari zaidi kujumuika na kikosi cha kusimamia usalama kilioko mjini Pibor chenye askari 80.

Mwaka jana maelfu ya watu wa kabila la Nur waliwashambulia Wamurle huko Pibor na kuuwa watu kama 150.

Mapigano kuhusu ng'ombe na wanawake yanatokea mara kwa mara Sudan Kusini.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.