Kamanda wa jeshi kizimbani I.Coast

Imebadilishwa: 2 Oktoba, 2012 - Saa 12:18 GMT

General Dogbo Ble (kulia) alikuwa mshirika wa rais wa zamani Laurent Gbagbo


Mshirika mkubwa wa rais wa zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo, amefunguliwa mashtaka mjini Abidjan, katika kesi ya kwanza ya watu waliotuhumiwa kwa ghasia za baada ya uchaguzi wa kati ya mwaka 2010 na 2011.

Generali Dogbo Ble alikuwa kamanda wa jeshi la Republican Guard chini ya uongozi wa bwana Gbagbo.

Yeye pamoja na maafisa wengine wa usalama wanatuhumia kwa mauaji ya kanali mmoja mkuu wa jeshi wakati wa mzozo huo uliodumu kwa miezi sita.

Bwana Gbagbo anasubiri kufunguliwa mashtaka katika mahakama ya kimataifa ya ICC. Anakana madai ya kuhusika na uhalifu wa kivita.

Ivory Coast imekuwa ikituhumu washirika wa Gbagbo, katika nchi jirani ya Ghana kwa kufanya uvamizi mipakani kwa lengo la kuitikisa serikali ya Rais Alassane Ouattara.

Mwandishi wa BBC John James anasema kuwa mahakama ilifurika watu kushuhudia kuanza kwa kesi ya Generali Dogbo Ble

Generali Ble, anayetoka kabila la bwana Gbagbo, aliibuka kama kamanda wa jeshi wakati wa vurugu la mwaka 2011 la kutaka udhibiti wa Abidjan, na kuendeshea harakati katika kambi ya muda iliyokuwa katika ikulu ya rais.

Alikuwa mmoja wa majenerali, ambao hawakumuunga mkono Rais Ouattara wakati wa kilele cha mapigano hayo.

Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wamepongeza hatua ya kumfungulia mashtaka kamanda huyo lakini wanaonya kuwa lazima kesi iendeshwe kwa usawa au la sivyo itaibua taharuki nchini humo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.