Shinikizo za Congress kuhusu Libya

Imebadilishwa: 3 Oktoba, 2012 - Saa 09:54 GMT

Wapiganaji nchini Libya

Bunge la Congress nchini Marekani limeongeza shinikizo kwa serikali ya Rais Obama kuhusu mashambulizi yaliyofanywa katika ubalozi wa Marekani mjini Benghazi.

Hii ni kufuatia ripoti kuwa jeshi linalenga wale waliohusika na shambulizi hilo.

Kamati moja muhimu imehoji ikiwa Marekani ilipuuza wito wa kuongeza ulinzi katika ubalozi huo.

Marekani ingali inafanya ujasusi kabla ya kile kinachosemekana kuwa operesheni ya kijeshi, dhidi ya wale waliohusika na mashambulizi hayo.

Hayati balozi, Christopher Stevens, balozi mwingine, Sean Smith na walinzi wawili walifariki kwenye shambulizi hilo ambalo lilitokea kufuatia ghadhabu katika nchi za kiisilamu baada ya kutolewa kwa filamu iliyokuwa inadhihaki dini ya kiisilamu na Mtume Mohammed.

Hata hivyo kuna maswala mengi ambayo yangali kujibiwa kuhusiana na mauaji hayo,

Serikali ya Marekani wiki jana ilisema kuwa baadhi ya waliohusika na shambulizi hilo ni watu wanounga mkono harakati za kundi la kigaidi la Al-Qaeda.

Namna ambavyo shambulizi hili lilishughulikiwa na serikali ya Marekani, imehojiwa vikali, huku Marekani ikijiandaa kwa uchaguzi wa urais.

Wanachama wa Republican wamekuwa wakikosoa serikali ya Rais Obama, kwa kulaumu filamu hiyo kuwa ndiyo iliyochochea mashambulizi wakati kulikuwa na njama ya mashambulizi ya kigaidi dhidi ya maslahi ya Marekani.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.