Uturuki yaidhinisha mashambulizi Syria

Imebadilishwa: 4 Oktoba, 2012 - Saa 14:29 GMT

Majeshi ya Uturuki mpakani na Syria

Bunge la Uturuki limetoa idhini kwa mashambulio ya kijeshi nje ya mpaka wake na Syria, iwapo hatua hiyo itahitajika na serikali. Hii inakuja baada ya Syria kufanya shambulizi kali dhidi ya Uturuki na kuwaua watu kadhaa.

Mswaada ulipitishwa na wabunge 320 na kupingwa na wabunge 129, pia inaruhusu mashambuizi dhidi ya maslahi ya Syria.

Hii inajiri saa chache tuu baada ya Uturuki kurejelea mashambulio ya kituo kimoja cha kijeshi cha Syria baada ya watu watano kuuwawa na mabomu ya Syria ndani ya Uturuki.

Naibu waziri Mkuu wa Uturuki Besir Atalay hata hivyo amesema idhini hiyo ya bunge sio hatua ya vita. Amesema Uturuki itachukua hatua hiyo kwa ushirikiano na taasisi nyingine zinazohusiana na mzozo wa Syria

Uturuki imekuwa ikifanya mashambulzi ndani ya Syria tangu siku ya Jumatano na kuwaua wanawake wawili na watoto watatu.

Kushambulia kwa makombora kwa Uturuki dhidi ya Syria na kuitisha kwake kwa mkutano wa dharura wa mabalozi wa mataifa wanachama wa NATO ni ilani tosha kwa Serikali ya Damascus.

Hii ni ishara kuwa uvumilivu wa Uturuki umefikia kikomo na kwamba Rais Bashar Al Asad atarajie kwamba Uturuki itaendelea kumshambulia mara kwa mara kuanzia leo.

NATO imeunga mkono kikamilifu Serikali ya Uturuki kama ilivyofanya mnamo Juni wakati makombora ya Syria yalipoangusha ndege ya Uturuki.

Kuna wakati ambapo Uturuki ilitaka kuwepo eneo nchini Syria ambako wakimbizi wa nchini humo wangeweza kupewa mahitaji bila kuingizwa Uturuki lakini dhana hii hawajaizingatia sana.

Wanachotaka hasa ni kushambulia Syria lakini kwa ushirikiano na NATO.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.