Wafungwa 20 watoweka Liberia

Imebadilishwa: 4 Oktoba, 2012 - Saa 14:08 GMT

Gereza

Takriban wafungwa 21 wametoroka gerezani Kusini Mashariki mwa mji wa Zwedru, nchini Liberia.

Kwa mujibu wa taarifa za redio ya taifa na maafisa wa utawala, zaidi ya wafungwa 60 walitoroka lakini msemaji wa polisi George Bardue ilikaridia wafungwa kuwa 21.

Aliongeza kuwa watoro hao ambao wamesemekana kuwa wamejihami, walifungwa jela baada ya kupatikana na hatia ya wizi na makosa mengine ya jinai.

Msako mkubwa unafanywa katika eneo la mpakani mwa nchi hiyo na Ivory Coast.

Eneo hilo ni hifadhi kwa maelfu ya wakimbizi waliotoroka vita nchini Ivory Coast baada ya vurugu zilizotokea kufuatia uchaguzi wa urais mwaka 2010.

Bwana Bardue alisema kuwa harakati zinafanywa kuwakamata wafungwa hao, waliotoroka hapo jana kutoka kwa gereza lenye ulinzi mkali la Zwedru.

Afisaa mkuu wa gereza hilo, Peter Solo, aliambia redio ya taifa kuwa zaidi ya wanaume 60 walitoroka, baadhi yao ambao wakiwa wahalifu sugu.

Aliongeza kuwa tahadhari imetolewa kwa maeneo ya migodi

Mwandishi wa BBC Jonathan Paye-Layleh mjini Monrovia, anasema kuwa, kama sehemu nyingi za vijijini nchini Liberia, Grand Gedeh nin jimbo ambalo kwa sasa haliwezi kufikiwa kwa urahisi kwa sababu ya barabara mbovu hasa wakati wa mvua.

Magereza katika nchi za Afrika Magharibi huwa yamesongamana kwa sababu ya kucheleweshwa kwa hatua za kisheria dhidi ya wafungwa.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.