Washukiwa wa mauaji wakamatwa Nigeria

Imebadilishwa: 4 Oktoba, 2012 - Saa 10:09 GMT
Chuo cha mafunzo anuwai cha Mubi

Polisi katika eneo la kaskazini mwa Nigeria wamesema wamewatia nguvuni washukiwa kadha kuhusiana na mauaji ya takriban watu 26 katika bweni la wanafunzi mjini Mubi.

Maafisa wa Serikali wanasema inaonekana waliouawa ni watu waliojulikana na kulengwa na wavamizi waliowatambua kwa majina.

Hapo awali ilishukiwa kuwa kundi la wapiganaji la, Boko Haram, lilihusika.

Hata hivyo, kiongozi mmoja wa zamani wa mwanafunzi ameiambia BBC kwamba huenda mauaji hayo yalichochewa na uhasama kati ya makundi ya wanafunzi yaliyoshiriki kwenye uchaguzi uliofanyika katika chuo kimoja cha mafunzo katika eneo hilo.

Ken Henshaw, aliyekuwa Rais wa Chama cha kitaifa cha Wanafunzi nchini Nigeria, amesema hakujawahi kufanyika uchaguzi wa wanafunzi bila kuwepo kwa umwagikaji wa damu tangu mwaka 2002.

Aliongezea kusema kwamba uchaguzi huo huchukuliwa kuwa ngazi ya kuelekea kwenye nyadhifa kuu za kisiasa Serikalini katika siku za usoni.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.