Wachimba migodi waandamana Afrika Kusini

Imebadilishwa: 6 Oktoba, 2012 - Saa 14:27 GMT

Mamia ya wachimba migodi wameandamana katika mji wa Rustenburg, Afrika Kusini, huku wakiimba.

Wachimba migodi nje ya migodi ya  kampuni ya Ango American

Wanawaunga mkono wenzao 12,000 ambao walifukuzwa makazini Ijumaa baada ya mgomo.

Polisi wengi wamewekwa mabarabarani.

Waandamanaji wamebeba mabiramu yakilaani kampuni inayochimba dhahabu nyeupe nyingi kabisa duniani, ya Anglo-American, kwa kuwatoa kazini wachimba migodi ambao wamekuwa wakigoma mara kadha.

Sekta ya migodi ya Afrika Kusini imekumbwa na migomo mingi siku za karibuni.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.