Mtumishi wa Papa ahukumiwa kifungo

Imebadilishwa: 6 Oktoba, 2012 - Saa 14:48 GMT


Mtumishi wa zamani wa Papa Benedict amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja na nusu kwa kuiba nyaraka za siri kutoka fleti ya Papa.

Paolo Gabrieli na Papa Benedict

Katika kujitetea mbele ya mahakama ya Vatikani, Paolo Gabriele alisema alifichua nyaraka hizo za siri kwa mwandishi wa habari kwa sababu akitaka kuonesha kile alichosema ni rushwa ovu ilioko katikati ya Kanisa la Katoliki.

Msemaji wa Vatikani, Federico Lombardi, alieleza kuwa inavoelekea Papa atamsamehe mtumishi wake.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.